Loading...

Monday, December 20, 2010

Steps entertainment Imeshaufunga mwaka.

Kampuni inayosambaza movie mbalimbali bongo ya Steps entertainment wiki iliyopita ilifanya party kubwa ya kufunga mwaka na kuwaalika wadau mbalimbali wa filamu nchini.Sherehe hii ilifanyika kigamboni katika hoteli ya Sunrise.


Watu wakijiachia ndani ya sherehe hizo

Baadhi ya wasanii wa filamu waliohudhuria sherehe hii

Safari ya Uzinduzi wa OFFSIDE

Hii ndio safari ya wakina kanumba kuelekea kongo kwenye uzinduzi wa filamu ya OFF SIDE


    Wakiwa Uwanja Wa Kimataifa wa ndege wa Mwl JK Nyerere


Wakiwa ndani ya ndege kuelekea kigali
Walipowasili Kigali Uwanja wa ndege


Washabiki wakiwfwata wasanii wa filamu ya Offside kutaka kuwaonaKanumba akihojiwa na waandishi wa Habari

Thursday, December 16, 2010

Kanumba na wenzake kama wafalme Kigali

iWasanii wa Filamu nchini Tanzania Kama Steven kanumba, Vicent Kigos, Ant Ezekiel na wenzao waliufunika mji wakigali kwa shangwe wakati wkiwasili na walipokuwa wakijivinjari mitaani. watu waliwafwata na kutaka kushikana nao mokono kuomba signature zao na hata kutaka kupiga picha pamoja. aaahii inaonyesha ni kwa jinsi gani fani ya uigizaji wa filamu tanzania umekuwa nje ya mipaka yetu, INAPENDEZA.Watu akiwa hawaamini kama wanaemuona ndio KANUMBA auUsipime hii ni ndani ya kigali

Habari hii ni kwa Hisani ya issamichuzi.blogspot.com

BORA NIFE hatimae ipo mitaani

Filamu iliyokuwa ina andaliwa na kampuni ya WHATEVER Film Production hatimaye imekamilika na sasa ipo madukani. Mkurugenzi wa kampuni hiyo bwana Hussein Mwaila alisema filamu hiyo ilianzakuwa madukani kuazia jana tarehe 15/12/2010. Moja ya wasanii walioigiza Filamu hiyo ya kuvutia ni Khadija Mohamedi aka Warda.  Blog ya Tollywood inawapa Hongera Whatever kwa kupiga hatua kubwa katika kukuza filamu nchini Tanzania. Na wewe unaesoma habari hii hakikisha unapata copy yako ya BORA NIFE original

Wednesday, December 15, 2010

GHONCHE MATEREGO AWAASA WASANII

Kusajili kazi za sanaa ni kuipa heshima Tasnia hiyo akitoa hoja hiyo katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Bwana Ghonche Materego wakati ea kikao cha nane cha utamaduni kinachoendelea mjini mwanza bwana Ghonche alisema.ni vizuri wadau wote wa sanaa hapa nchini wakasajili kazi zao. Kusajili kutaifanya sanaa kuheshimika na kujulikana sehemu tofauti duniani na si kudharauliwa kama ilivyo sasa.

JB atoa ushuhuda kwa waziri Nchimbi

Msanii wa filamu maarufu hapa nchini bwana James Michael alitoa ushuhuda wa mafanikio yake na TASNIA ya Filamu nchini kwa ujumla mbele ya waziri wa Habari,Utamaduni,Vijana na Michezo Dkt Nchimbi katika kikao cha nane cha kazi cha utamaduni kilichofanyika mjini mwanza.

Tuesday, December 14, 2010

Kanumba na Uncle JJ, Ray na Family Disaster Hapatoshi

Manguli wa Filamu nchini Tanzania Kanumba na Ray wanafunga mwaka kwa kutupa kazi zao sokoni. Huku kanumba akichomoka na UNCLE JJ, Ray yeye amedondosha Familiy Disaster. Kama haitoshi wote kwa pamoja wanaandaa Filamu nyingine iitwao OFFSIDE watakayo washirikisa Irene Uwoya.
posta ya UNCLE JJ kama inavyonekanaKanumba na Ray Ndani ya OFFSIDE

Na Hii imeletwa kwenu kwa msaada mkubwa wa Blog ya kanumbathegreat.blogspot.com