Monday, December 20, 2010

Steps entertainment Imeshaufunga mwaka.

Kampuni inayosambaza movie mbalimbali bongo ya Steps entertainment wiki iliyopita ilifanya party kubwa ya kufunga mwaka na kuwaalika wadau mbalimbali wa filamu nchini.Sherehe hii ilifanyika kigamboni katika hoteli ya Sunrise.


Watu wakijiachia ndani ya sherehe hizo

Baadhi ya wasanii wa filamu waliohudhuria sherehe hii

Safari ya Uzinduzi wa OFFSIDE

Hii ndio safari ya wakina kanumba kuelekea kongo kwenye uzinduzi wa filamu ya OFF SIDE


    Wakiwa Uwanja Wa Kimataifa wa ndege wa Mwl JK Nyerere


Wakiwa ndani ya ndege kuelekea kigali




Walipowasili Kigali Uwanja wa ndege


Washabiki wakiwfwata wasanii wa filamu ya Offside kutaka kuwaona



Kanumba akihojiwa na waandishi wa Habari

Thursday, December 16, 2010

Kanumba na wenzake kama wafalme Kigali

iWasanii wa Filamu nchini Tanzania Kama Steven kanumba, Vicent Kigos, Ant Ezekiel na wenzao waliufunika mji wakigali kwa shangwe wakati wkiwasili na walipokuwa wakijivinjari mitaani. watu waliwafwata na kutaka kushikana nao mokono kuomba signature zao na hata kutaka kupiga picha pamoja. aaahii inaonyesha ni kwa jinsi gani fani ya uigizaji wa filamu tanzania umekuwa nje ya mipaka yetu, INAPENDEZA.



Watu akiwa hawaamini kama wanaemuona ndio KANUMBA au



Usipime hii ni ndani ya kigali

Habari hii ni kwa Hisani ya issamichuzi.blogspot.com

BORA NIFE hatimae ipo mitaani

Filamu iliyokuwa ina andaliwa na kampuni ya WHATEVER Film Production hatimaye imekamilika na sasa ipo madukani. Mkurugenzi wa kampuni hiyo bwana Hussein Mwaila alisema filamu hiyo ilianzakuwa madukani kuazia jana tarehe 15/12/2010. Moja ya wasanii walioigiza Filamu hiyo ya kuvutia ni Khadija Mohamedi aka Warda.  Blog ya Tollywood inawapa Hongera Whatever kwa kupiga hatua kubwa katika kukuza filamu nchini Tanzania. Na wewe unaesoma habari hii hakikisha unapata copy yako ya BORA NIFE original

Wednesday, December 15, 2010

GHONCHE MATEREGO AWAASA WASANII

Kusajili kazi za sanaa ni kuipa heshima Tasnia hiyo akitoa hoja hiyo katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Bwana Ghonche Materego wakati ea kikao cha nane cha utamaduni kinachoendelea mjini mwanza bwana Ghonche alisema.ni vizuri wadau wote wa sanaa hapa nchini wakasajili kazi zao. Kusajili kutaifanya sanaa kuheshimika na kujulikana sehemu tofauti duniani na si kudharauliwa kama ilivyo sasa.

JB atoa ushuhuda kwa waziri Nchimbi

Msanii wa filamu maarufu hapa nchini bwana James Michael alitoa ushuhuda wa mafanikio yake na TASNIA ya Filamu nchini kwa ujumla mbele ya waziri wa Habari,Utamaduni,Vijana na Michezo Dkt Nchimbi katika kikao cha nane cha kazi cha utamaduni kilichofanyika mjini mwanza.

Tuesday, December 14, 2010

Kanumba na Uncle JJ, Ray na Family Disaster Hapatoshi

Manguli wa Filamu nchini Tanzania Kanumba na Ray wanafunga mwaka kwa kutupa kazi zao sokoni. Huku kanumba akichomoka na UNCLE JJ, Ray yeye amedondosha Familiy Disaster. Kama haitoshi wote kwa pamoja wanaandaa Filamu nyingine iitwao OFFSIDE watakayo washirikisa Irene Uwoya.




posta ya UNCLE JJ kama inavyonekana



Kanumba na Ray Ndani ya OFFSIDE

Na Hii imeletwa kwenu kwa msaada mkubwa wa Blog ya kanumbathegreat.blogspot.com

Filamu Ya BABU SEYA bado ipoipo

Filamu inayokwenda kwa jina la BABU SEYA imekwama kuingia sokoni kutokana na Msambazaji wa Filamu hiyo kushauri baadhi ya vitu vipunguzwe kwenye Filamu hiyo. Mratibu wa Filamu hiyo Octavias amesema bila shaka baada ya kumalizika kufanyiwa marekebisho hayo itakuwa sokoni.
Msambazaji wa Filamu Hiyo alishauri kupunguzwa baadhi ya vitu ili kuepusha matatizo pindi itakapotoka.

Mzee KIpara Ana SHINE kama kawa

Mzee kipara ameanza kuonekana katika shughuli mbalimbali za sanaa na anaonekana kuimarika kiafya.
Mzee Huyo ambae ni moja ya wakongwe wa sanaa ya tasnia ya maigizo na filamu alikuwa anaugua kwa muda mrefu lakini kwa sasa anaonekana kuwa na afya njema baada ya kushine katika harusi ya CHIKI msasani club. NJOO MZEE WETU TULIKUMIS SANA



Mzee kipara akionyesha some LOVE katika Harusi ya Bwana CHIKI

Rita Dominic ataka kuihudumia Jamii Ya KItanzania

Msanii wa Filamu Nchini Nigeria ameomba kufanya kazi za kijamii pindi atakapokuwa nchini wakati wa uzinduzi wa Shindano la Filamu hapa nchini.

Akizungumza na Jukwaa la sanaa BASATA rais wa shirikisho la Filamu nchini Bwana SIMON MWAKIFAMBA alisema wakati anawasiliana na Rita, Rita alikubali mualiko huo na kusema ni heshima kubwa amepewana jamii ya Tanzania hivyo kuirudishia fadhila alioba ahusishwe kwenye shuhguli za kijamii atakapokuwa nchini. Rita aliomba Ratiba na Kazi za kijamii. Karibu sana RITA DOMINIC TANZANIA

Kanumba ashusha shoo ya ajabu

Msanii wa Filamu nguli nchini Steven Kanumba The Great ama ukipenda mwite Uncle JJ alishusha shoo ya hatari na wenzake katika harusi ya mwenzao CHIKI katika ukumbi wa Msasani Beach CLub Makuti.
Ebwana alishusha shoo matata kama Madilu System.



KAnumba akimwaga Shoo


Director Ramadhani Kingalu alalamikia waandishi

Director wa Filamu wa siku nyingi hapa mjini bwana Ramadhani Kigalu amewalalamikia waandishi wa habari wanaotafuta mabaya tu na kuyaandika na kusahau kuandika mazuri wanayo yafanya wasanii wa filamu hapa nchini. Akizungumza katika Jukwaa la sanaa linalofanyika kila siku ya jumatatu katika ukumbi wa  baraza la sanaa BASATA  bwna Rama alisema "kuna baadhi ya waandishi kazi yao kutafuta mabaya tu katika kazi zetu tukifanya mazuri hawaandiki hii inafanya kutudidimiza sana sisi wasanii kwenye Tasnia yetu"

JOYCE KIRIA ni bibi harusi mtarajiwa

 mkurugenzi wa local movies entertainment JOYCE KIRIA ambaye pia ni mtangazaji wa clouds fm lAmeanza safari ya maandalizi ya harusi ya ke inaytarajiwa kufanyika hivi karibuni. ahabari zilizopatikana katika blog yake zinasema vikao vya kitchen party vinaendelea katika Club ya ROSTERS PUB.mikocheni. Blog ya Tollywoodleo inakupongeza Joyce kwa maamuzi ya busara maana ndoa ni tendo jema.


JOYCE KIRIA

CHIKI apata JIKO


Msanii wa Filamu nchini SALUMU MCHOMA maarufu kama CHIKI alifunga ndoa na kuuaga ukapela mwishoni mwa wiki iliyo pita.

Bwana Chiki alifunga ndoa nyumbani kwa wazazi wa bibi harusi Bi Zuhura na baadae harusi ilifana kwa sherehe kabambe iliyofanyika katika ukumbi wa Makuti Msasani Beach CLub. Blog Ya TollywoodLeo Inawatakia maisha mema na yenye fura Chiki na Mkewe Bi Zuhura.

TOLLYWOODLEO "get to know everything about bongo movies"

[irene.jpg]
Malkia wa Filamu nchini Irene Uwoya


Wapenzi wa sanaa ya filamu nchini Tanzania kuazia sasa watakua wananafasi nzuri ya kujua kwa karibu habari zinazohusu tasnia hiyo hapa nchini baada ya BLOG maalum kwa ajili ya habari za tasnia hiyo kufunguliwa na mwanahabari mkereketwa wa sanaa nchini Bwana Prosper William.

Mwanahabari huyo amesema ameamua kufungua blog hiyo kutokana na kuwepo vombo na vipindi vichache sana vinavozungumzia tasnia hiyo inayopendwa sana hapa nchini. Katika Blog hiyo kutakuwa na mambo mbalimbali kuhusu wasanii, maproducer,madirector, wasambazaji, na wateja wa tasnia hiyo.

Akizungumza wakatiwa mahojiano na blog hii Bwana Prosper alisema mambo yataongelewa kiundani sana ili kuwapa watazamaji fulsa ya kuitambua tasnia hiyo kiundani na kuipenda tofauti na vyombo vingine vinavyoichukulia tasnia hiyo.